Dondoo za masuala ya usajili zimekuwa zikimuhusisha Neymar na kusepa PSG akionekana ameshachoshwa na mshike mshike wa Ligue 1. Neymar alikuwa anahusishwa sana na klabu ya Real Madrid na klabu yake ya zamani ya Barcelona. Taarifa zinadai kuwa Neymar amepewa masharti kadhaa ikiwa anataka kurejea Barca.

Taarifa zinadai kuwa staa huyu alichagua kurejea Barcelona kuliko kwenda Real Madrid. Neymar akiwa PSG, katika msimu uliopita alikukutana na kipindi kigumu sana, pengine ni kigumu zaidi katika soka lake la kulipwa baada ya kupata mikiki mikiki ya majeraha na kujikuta akitumia mda mrefu nje ya uwanja.

Klabu ya Barca, waliripotiwa kuwa wapo tayari kumpokea kijana wao ambaye pia amekiri kuwa kuondoka klabuni hapo ilikuwa ni kosa. Lakini ili aweze kurejea kuivaa jezi ya Barcelona, moja ya masharti ambayo ni lazima akubaliane nayo ni kupungua kwa mshahara.

Soko la uhamisho wa wachezaji linatarajiwa kupigwa vibaya na janga lililoikumba ulimwengu ambalo kwa nafasi yake limeleta athari kubwa katika ulimwengu wa soka na uchumi wa vilabu.

PSG wanajiandaa kumbakiza Neymar na mwenzake Kylian Mbappe na wapo tayari kujitahidi kuwapa kile watakachohitaji. Ikiwa mastaa hawa wataondoka kwa namna yeyote PSG, lazima watakuwa wamepata ofa nzuri zaidi, je ni klabu gani kwa hali ya sasa ipo tayari kuwalipa mishahara mikubwa wanayolipwa PSG ukiacha ada zao za uhamisho?

Kiuhalisia klabu ya Barcelona haifanani na klabu ya PSG kiuchumi, PSG wakitajwa kuwa na pesa zaidi, hivyo Barcelona hawataweza kumlipa Neymar malipo yale yale aliyokuwa akilipwa na PSG.  Hivyo kupunguzwa mshahara ni kipaumbele ili staa huyu aivae jezi ya La Liga tena! Ungekuwa yeye?

Barcelona wanamuhitaji nyota huyu pia kukubali kutolipwa baadhi ya bonasi. Wadau wanaamini huenda staa huyu akarejea relini kama akirejea Barcelona kwa sababu ya uwepo wa Messi Barcelona, wawili hawa wanaiva sana wakiwa pamoja.

46 MAONI

  1. Bora aende epl kuliko kwenda laliga epl Kuna timu kibao zinamuitaji pia atokutana na hayo makato yote na atakuwa mchezaji wakuangaliwa muda wote

  2. Bora aende epl kuliko kwenda laliga epl Kuna timu kibao zinamuitaji pia atokutana na hayo makato yote na atakuwa mchezaji wakuangaliwa muda wote#meridianbettz

  3. Inavyoonekana Barcelona hawamuhitaji kama wangemuhitaji wangekubaliana mshahara kwa sababu ya kiuchumi lakini kuweka mashariti sio sahii

  4. Kwa kiwango chake kwa Sasa ni Bora tu angekubali kupunguziwa mshahara Barca akifanya vizuri na Barca Bado wakiwa wanamuhitaji ataongezewa tu.

  5. Nimekuwa nikishuhudia maamuzi mengi mabaya ya wachezaji wa Brazil wakati wa usajiri. kama Neymar hajapata alilotaka akiwa PSG sioni maajabu atakayopeleka Barcelona.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa