Ryan Mason amepewa majukumu ya muda mfupi ya kuwa kocha wa Tottenham mpaka mwisho wa msimu huu baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho.

Mason Kuimeneji Tottenham Mpaka Mwisho wa Msimu

Spurs walimfungishia virago Mourinho siku ya Jumatatu siku sita kabla ya fainali ya kombe la EFL Cup dhidi ya Manchester City huku tumaini la kufuzu Ligi ya Mabingwa likiwa shakani.

Mchezo wa kwanza atakabiliana na Southampton katika Premier League siku ya Jumatano.

Mason atasadiana na Chris Powel na Nigel Gibbs pamoja na Ledley King ataendelea kuwa msaidizi wa timu ya kwanza na Michel Vorm atakuwa kocha wa makipa.

Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy alizungumzia kiwango na ubora wa klabu baada ya kuthibitisha kuchaguliwa kwa Mason siku ya Jumanne.

“Tuna imani kubwa na kikosi hiki ambacho kinawachezaji wenye vipaji,” alisema.

“Tupo kwenye fainali na tumesaliwa na mechi sita katika Premier League kwa sasa itatupasa kuangalia nguvu zetu na kufanikisha msimu kwa ukubwa.

Mason miaka 29, alikuwa mchezaji wa Spurs kwa muda wa miaka 8 baada ya kutokea kwenye akademi ya klabu.

Baadaye alijiunga na Hull City lakini alipata jeraha la fuvu mwezi Januari mwaka 2017 mwishowe alilazimika kustaafu kucheza soka na akahamia kwenye ukocha na Spurs mwaka 2018.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Mason, Mason Kuimeneji Tottenham Mpaka Mwisho wa Msimu, Meridianbet

CHEZA HAPA

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa