Massimiliano Allegri anaripotiwa kukataa nafasi ya kuwa mkufunzi mkuu mpya wa Tottenham Hotspur.
Klabu ya London Kaskazini inatafuta mbadala wa Jose Mourinho, na bwana huyu ametajwa kama mmoja wa wanaohusishwa na kuchukua nafasi hiyo katika uwanja wa Tottenham Hotspur.

Bosi huyu wa zamani wa Juve, mwenye miaka 53 hajawa kazini tangu alipoondoka Juventus msimu wa joto wa 2019, lakini meneja huyo mwenye uzoefu anaendelea kuhusishwa na vilabu kadhaa vinavyoongoza Ulaya.
Massimiliano Allegri Aikana Spurs

Kwa mujibu wa AS, Tottenham hivi karibuni iliwasiliana na Allegri juu ya uwezekano wa kuchukua jukumu la kazi Spurs, lakini Muitaliano huyo alikataa habari hiyo.

Ripoti hiyo inadai kwamba mshindi huyo wa mara sita wa Serie A anamngojea Zinedine Zidane afanye uamuzi juu ya hatma yake na Real Madrid kabla ya kupanga mipango yake mingine.

Zidane anadaiwa kuwa anaweza kuondoka Los Blancos mwishoni mwa msimu, na Allegri anasemekana kutazamwa na mabingwa wa Uhispania kama mbadala wa Mfaransa huyo.

 

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa