Huu ni msimu ambao Formula 1 inanogeshwa na ushindani mkali kati ya Max Verstappen na Lewis Hamilton, hapa ni timu Red Bulls vs Mercedes. Noma na nusu!

Wikiendi hii kutafanyika mashindano ya mbio za Monaco GP kule nchini Ufaransa, Verstappen na Hamilton wamekuwa wakichuana vikali katika mbio nne zilizofanyika mpaka sasa kwenye kalenda ya F1.

Wawili hawa wamekuwa wakimaliza kwenye nafasi ya 1 na 2 huku Hamilton akiwa tayari ameshinda mbio 3 kati ya 4 walizocheza mpaka sasa. Baada ya kuchuana vikali, Lewis Hamilton alinukuliwa akisema ” nadhani nimefanya vizuri kwenye kuzuia migusano. Lakini bado tunambio 19, tunaweza kukutana. [Max Verstappen] Anajihisi labda anakitu cha kuthibitisha. Sipo sawa nae kwenye jahazi hilo.”

Verstappen amejibu usemi huo kutoka kwa mpinzani wake, kwa mujibu wa dereva huyu “Sina cha kuthibitisha. Kuzuia migusano ni suala la pande zote mbili, tumepambana sana na tumejitahidi kuzuia migusano kwa pande zote. Tuna imani tunaendelea kufanya hivyo na kuchuana vikali.”

Huu ni msimu ambao Hamilton anaitafuta rekodi ya dunia kwa kubeba taji la 8 kwenye F1 akiwa na timu ya Mercedes. Mpaka sasa, Hamilton anamzidi Verstappen kwa pointi 14 baada ya mbio 4 za mashindano.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Max Verstappen, Max Verstappen, “Sina Cha Kuthibitisha”., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa