Nyota wa PSG, Kylian Mbappe ameripotiwa kuwa amemwambia Mauricio Pochettino kuwa hana mpango wa kuendelea kuwepo klabuni hapo zaidi ya mwaka 2022. 

Mkataba wa nyota huyu, mshindi wa Kombe la Dunia unaisha mwakani, maana yake miski ujao wa joto 2022 anaenda kuwa mchezaji huru.

Taarifa zinataja kuwa PSG sasa wanamlenga mwanatimu mwenziwe wa timu ya taifa, Paul Pogba wakati nyota huyu wa miaka 22 akihusishwa zaidi na Real Madrid.

Kwa mujibu wa Marca, baada ya likizo ya kimataifa, Mbappe amemwambia meneja Pochettino kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba wa kusalia klabuni hapo.

Wakati nyota huyu akiwa amejiandaa kuwa na subira, bila kuharakisha uhamisho wake Real Madrid wanapata nafasi ya kujiandaa na kufanya maamuzi ya kuwasilisha ofa rasmi.

Mbappe amehusika moja kwa moja na magoli 193, akifunga 132 na kutoa asisti 61 kwenye mechi 171 alizocheza kwa misimu minne pale PSG.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa