Juni 28 2021 itakuwa ambayo Kylian Mbappe ataikumbuka kwa muda mrefu, baada ya bahati mbaya ya kukosa penati dhidi ya Switzerland kumuangukia na Ufaransa kuondolewa lwenye michunao ya Euro 2020  siku ya Jumatatu usiku.

Mbappe Atoka Kapa Michuano ya Euro 2020

Hakuna hata penati moja iliyokosa katika mikwaju ya penati, na Mbappe akapiga penati ya tano ya Ufaransa. Wakati mshambuliaji huyo akirudi nyuma, kulikuwa na hali ya kutokuwa na uhakika kwenye uso wa mchezaji, mchezaji ambaye alikuwa amechangia sana wakati wa dakika 120.

Aliingia kwenye mashindano kama nyota anayeweza kuwa kiwango maridadi kwenye mashindano na aliondoka kwa kilio wakati timu yake ilitolewa kutoka raundi ya 16.

Mbappe alishindwa kufunga bao hata moja ambalo halikuwa la kuotea katika mashindano, licha ya kupata nafasi chache za wazi wakati wa mashindano. Mchezaji pembeni yake, Karim Benzema, alimaliza mashindano hayo kwa mabao manne.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alizungumza baada ya kuondolewa kwa timu yake, akijutia kukosa kwake.

“Ni ngumu sana kumaliza, huzuni ni kubwa baada ya kuondolewa huku kwani hatukuweza kufikia lengo letu,” alisema.

“Nimevunjika moyo kwa kukosa penati hiyo, nilitaka kuisaidia timu lakini nilishindwa.

“Kulala itakuwa ngumu usiku wa leo, lakini ni heka heka za mchezo huu ambao naupenda sana.”

“Najua mashabiki wamekata tamaa, lakini nataka kuwashukuru kwa msaada wao na kwa kutuamini kila wakati.”

“Hongera Uswizi.”


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa