Mbappe hajaona juu ya nani anaweza kumchagua na nani amuache kwa nafasi zao kama wachezaji bora wa dunia kati ya Messi na Ronaldo. Kwake yeye wawili hao ni bora zaidi na kila mmoja anafanya makubwa kwa nafasi yake na kila mmoja ni bora kwa mwenzake kwenye eneo fulani ambalo mwingine haliwezi hilo eneo.

Kwake yeye anaona ni bora akae pembeni kabisa ili kuwaacha wawili hao waweze kufanya makubwa kuliko yeye kujihusisha kwenye kundi hilo. Anasema ni bora yeye akae pembeni kabisa na kuwapa nafasi Messi na Ronaldo waingie uwanjani na timu yake ikapata ushindi kuliko kuchagua kwa kusema mmoja wao yupo bora zaidi ya mwingine.

Nyota huyo wa Barcelona alikuwa katika kiwango cha pekee kupata ushindi mbele ya Manchester United baada ya kufumania nyavu mara mbili na kuwaacha United wakiwa hawana la kufanya mbele ya wababe hao waliokuwa mbele ya mashabiki zao wengi sana. Kwa hakika alikuwa katika uwezo wa kipekee sana.

Lakini pia upande wa pili, Juventus walishindwa kutamba wakiwa nyumbani mbele ya Ajax ambao walikuwa kwenye ubora wao wa hali ya juu. Pamoja na Ronaldo kuwapa Juventus uongozi kwa goli lake la mapema sana ndani ya mechi yao hiyo. Na kuwafanya Ajax kupigana kwa kasi ya ajabu kutafuta ushindi kwa nguvu.

Pamoja na kutimka ligi yake hiyo aliyoizoea kwa kipindi kirefu lakini ameweza kufanya kubwa zaidi ndani ya ligi hiyo ambayo ni msimu wa pili pekee tangu ajiunge nayo.

Kwa hakika siyo rahisi kuweza kuwatenganisha wawili hao kutokana na sifa za nje tu ambazo mtu anazifikiria; kwa maana hiyo wawili hao kuna haja ya kuwatofautisha na kuwafananisha kwa vigezo pekee ambavyo vinaweza kuwa bora zaidi na kwamba kila mmoja anaweza kufanya analojisikia kwa wakati wake. Siyo rahisi kukurupuka tu na kusema mmoja ni bora zaidi ya mwingine kwa wepesi tu.

Messi naye hayupo mbali kwenye ubora wake katika kampeni zake za kisoka. Hizo ni takwimu kubwa na nzuri kwa nyota huyo kuweza kuzifikia kwa msimu pekee; siyo rahisi kwa mchezaji kuweza kufikia hatua hiyo ndani ya msimu pekee na kutokana na hilo basi, ni uwezo mkubwa sana wa mchezaji unapimwa kupitia hilo.

Naamini wengi wataungana na Mbappe kwa uchaguzi huo wa kuweza kujiweka wao pembeni na kuwaweka wawili hao kwenye nafasi zao ili basi kuwaacha wapambane uwanjani ili timu iweze kupata matokeo sahihi kwa wakati sahihi; zaidi ya kuhangaika kuwafananisha na kuwatofautisha kwa uwezo wao.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa