Klabu ya Manchester United tayari wanaripotiwa kuwasilisha ofa rasmi ya Kumrejesha Cristiano Ronaldo pale Old Trafford.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali kutoka Uingereza na Italia, Manchester United wamewasilisha ofa rasmi kwa Jorge Mendes juu ya uwezekano wa kupatikana kwa nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo.

Uvumi juu ya mpango huu wa United umeenea sana wiki hii baada ya Juventus kudaiwa kuwa wapo tayari kumuachia nyota huyu wa miaka 35 katika dirisha lijalo la msimu wa joto ikiwa ni jitihada za kupunguza gharama za mishahara.

Wakati huo, taarifa nyingine kutoka Ufaransa zinasema kuwa Paris Saint-Germain, tayari wameshathibitisha kwamba watakuwa tayari kuchukua hatua juu ya staa huyu.

Ronaldo aliondoka United kwenda Real Madrid mnamo 2009, kisha akahamia Juventus na sasa mashetani wekundu wanamuhitaji arejee tena Old Trafford.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa Ronaldo anaifikiria ofa ya United licha ya kuendelea kuzingatia msimu wake uliobaki na Juventus.

Lakini, suala la hili bado linaweza kuwa gumu kidogo kwa United kumnasa Ronaldo, ukizingatia  Woodward tayari alielezea hali ya Klabu hiyo baada ya athari za janga la Corona.

Ripoti zingine nchini Uhispania zinadai United wanataka kuwasaini wote wawili Eduardo Camavinga na Erling Haaland msimu ujao wa kiangazi.


 

UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

25 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa