Katika dunia hii kila mtu ana uwezo flani katika kitu anacho kifanya na ndio maana David Beckham ni mmoja ya wachezaji wachache sana wenye uwezo mkubwa wa kupiga mipira ya Adhabu (Fauls ) Uwezo wa Becham kwenye Kupiga Mipira mingi ya Faul ni wa ajabu mno.

Hebu Jiulize Mtu anapiga Mpira kati kati ya mabeki watatu mpaka sita waliotengeneza ukuta ili kuzuia mpira na unawapita, Hiyo haitoshi unavuka pia mlinda mlango na kuchezesha nyavu za wapinzani wake, na hii si kwa mara moja ilikua ni kila alipopata nafasi ya kupiga mipira ya fauls.
Story zisizo rasmi zinasema mwamba David Beckham alikua akifika mazoezini alikua anatenga muda wa ziada kujifunza kupiga fauls na alikua anajua hasa kwa maana alitenga mipira kadhaa mbali na goli na kuhakikisha mipira yote inagonga nguzo, Hizi hazina uhakika ila Uhakika unakuja pale anapokua uwanjani na kuonesha kua huyu mtu si wa kawaida.
Kuupiga mpira kwa miguu yote iwe wa kushoto au wa kulia ni uwezo wa ajabu sana, Unaweza kusema huyu mwamba miguu yake ina macho au laa. Uchambuzi huu haujagusia rekodi halisi za kitaalamu na takwimu ila tuna ahidi kurudi na rekodi rasmi za magoli ya faul ya David Beckham
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Magdalena
Beckam alikuwa vizuri