Mshambuliaji Prince Dube, anakuwa mchezaji wa kwanza wa Azam FC kufunga mabao 13 kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), baada ya staa wa zamani, Kipre Tchetche
Tchetche ndiye aliyekuwa mchezaji wa mwisho wa Azam FC kufunga jumla ya mabao 13 kwenye ligi, akifanya hivyo msimu ambao Azam ilibeba ubingwa wa ligi 2013/2014.
Dube aliyesajiliwa na Azam msimu huu, hadi sasa ndiye kinara wa ufungaji mabao kwenye ligi, baada ya kutikisa nyavu mara 13.
Zikiwa zimesalia mechi tano za ligi ili kukamilisha msimu huu, Dube anayo nafasi kubwa kuongeza mabao na kuitafuta rekodi ya klabu kwa msimu ambayo ni mabao 19, inayoshikiliwa na John Bocco tangu msimu wa 2011/12.
Vilevile yupo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa VPL msimu huu.
Azam FC hadi sasa ikicheza msimu wake wa 13 tokea ipande daraja mwaka 2008, imefanikiwa kutoa wafungaji watatu bora, mara 3 mfululizo kwenye ligi.
2010/11 Mrisho Ngassa – mabao 16
2011/12 John Bocco – mabao 19
2012/13 Kipre Tchetche – mabao 17.
REKODI NDANI YA KLABU
Msimu wa kwanza tunacheza Ligi Kuu 2008/2009, mfungaji bora wa klabu alikuwa Nsa Job, aliyefunga mabao tisa, huku msimu 2009/2010 akiwa Bocco baada ya kufunga mabao 14.
Ngassa, Bocco na Tchetche wakafuatia misimu iliyofuata (2010/2011, 2011/2012, 2012/2013), ambayo waliibuka wafungaji bora kwenye ligi pia.
Tchetche akawa mfungaji bora tena wakati Azam inabeba ubingwa wa ligi 2013/2014 akifunga 13, huku Didier Kavumbagu, akiwa mfungaji bora wa Azam msimu 2014/2015 kwa mabao yake 10.
Wafungaji wengine;
2015/16 | Kipre Tchetche | 12 ⚽
2016/17 | John Bocco | 9 ⚽
2017/18 | Shaaban Chilunda | 10 ⚽
2018/19 | Donald Ngoma | 11 ⚽
2019/20 | Obrey Chirwa | 12 ⚽
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Sadick
Ligi yetu imeanza kutawaliwa na wafungaji wa nje, kuna haja wabongo kukaza buti zaidi kuleta ushindani zaidi kuwania kiatu cha dhahabu