Klabu ya Hispania FC Barcelona Imemtimua kocha wao, Quique Setien siku tatu baada ya kuingoza Klabu hiyo kuchapwa 8-2 na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa,Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman ambaye alichezea kwa miamba hao wa Kikatalani kati ya 1989 na 1995, amepanga kuchukua nafasi ya Setien huko Camp Nou.
Meneja wa zamani wa Real Betis Setien, 61, aliteuliwa mnamo Januari na kuiongoza Barça katika mechi 25 tu – Barca ilimaliza ha pili katika La Liga msimu huu, alama tano nyuma ya Mabingwa Real Madrid na Kocha mpya atatangazwa “katika siku zijazo,” ilisema Klabu hiyo.

Aliajiriwa kama kocha wa Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili na nusu kama mbadala wa Ernesto Valverde mwaka 2020 mwezi Januari.
Mwezi Januari Anashinda mchezo wake wa kwanza baada ha Lionel Messi kufunga bao la pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Granada.
Mwezi Februari, Anaiongoza klabu kutolewa kwenye Copa del Rey katika hatua ya robo fainali mbele ya Athletic Bilbao.
Mwezi Machi 1 Alipoteza El Clasico vs. Real Madrid, ambao rasmi waliongoza msimamo ajuu ya Barcelona kileleni mwa La Liga.
Julai 16 Barca inapoteza rasmi matumaini ya taji la La Liga kwa kupoteza mchezo wao wa nyumbani baada ya kutopoteza mechi 30 – Osasuna wakishinda 2-1 huko Camp Nou.
Agosti 14, 2020: Inapoteza kwa kipigo cha rekodi ya Klabu 8-2 mbele ya Bayern Munich na kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa kwenye mchezo wa robo fainali.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


magdalena
bora wamemtimua maana alijisahau katika majukumu yake ya kupanga kikosi kizuri
Ester jackson
Barcelona kumuondeo kucha pekee bado haitoshi wafanye mabadiliko bodi zima inayo simamia klabu hiyo
Ester jackson
Barcelona kumuondoa kocha pekee bado haitoshi wafanye mabadiliko bodi zima ya klabu hapo
rama
Maoni:atapata timu nyingine tu barcelona timu kubwa inaitaji matokeo chanya tu
Ernest
Tunaweza mlaumu Kocha lakini ki ukweli Barca ya sikuhizi imeoza, ila Quique Setien pia hakuwa na nyakati nzuri ndani ya Barca
Dorophina
Kumfukuza kocha sio sababu inabidi wakae chini wajue tatizo nn
felister
sidhani Kama kumuondoa kocha ndo kutatua tatizo inabidi wakae watafakari wapi wamekosea
Furahav
Ama kweli kazi ya ukocha ngumu sana.
Caroline
Atapata Timu nyingine
Gabriel
Quique Setien ni kocha mzur sana 👍 me naamin tatizo la kufungwa ni jambo la bahat mbaya sana aina maana kuwa kocha ndo mzembe bal ilikuwa wachezaji hawakuwa katika position nzur hiyo ndo sababu kubwa
Neema
Kwahy kumwondoa ndio watakuwa wametatua tatizooo?
farida ahmadi
Kikubwa ni kikosi chenyewe kujiweka sawa
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli Barcelona imebugi kumuondoa Setien ndio kufanya vizuri akuna kitu kamaicho Setien nikocha mzuri Ila haikukaa levo inayo takiwa ndomana ikashuka kimchezo nakufungwa nikawaida tuu sio kilasiku mpate atasiku moja moja mkiachia sio mbaya
Nasra
Wajiweke sawa tu hakuna namna
Antony Luseno
Msimu huu barca wamekuwa na matokeo mabaya sana
Tatu
Wafanye hesabu za toa na kuzidisha ili timu ikae sawa
Hope mwaikuka
Malizanen tu kwa aman
Edgar
Aya ngoja tuone msimu ujao kama msimu huu tatizo kocha
Sauda
Ukocha kazi ngumu sana
Sabrina
Kumuondoa kocha sio tatizo wanatakiwa waangalie walipo jikwaa
Zeiyana
Daaah..!kwaiyo Barcelona waona tatizo lipo kwa kocha..!haya suburi tuone mwisho wake
Fatuma kasomo
Ukocha kz sana
Shafii
Kwa matokeo ya setien kwenye ile mechi hata ningekua Mimi bosi wa barca ningekipiza.
Theonestina
Apambane tu maisha popote
Issa
Bayern wamewafanya wenzao vibaya
Povel
Kocha wamembebesha zgo la lawama kiukwl Barca fc wapo kwny ubora tuliohuzoeh hule
JULIANA
Da! Ukocha ni shida mwanawane
Janeflora malisa
Kaz begum sana ya ukoch
Janeflora malisa
Kaz ngum sana ya ukocha
Samiah
Ukocha nikazi ngumu
Latifa juma mohamed
Seitene ni kocha mzur, Bayern wamefel kwa kutoangalia wapi wamejikwaa ,ni vema na vzr wangeund kikosi upya ,asijal maisha popote.
Mwanahamisi
Bayern wamewafanya wenzao vibaya
Khadija
Barcelona kumuondoa kocha pekee itakuwa haitoshi inabidi wafanye mabadiliko ya bodi nzima
aisha
Barcelona kuweni makini sana msije mkafeli tena
Mwajumah
Atapata team nyingine
Fatina mfingi
Barcelona wantakiwa kuwa Makin San!
David Pere
Tunaweza mlaumu Kocha lakini ki ukweli Barca ya sikuhizi imeoza, ila Quique Setien pia hakuwa na nyakati nzuri ndani ya Barca
Saupha mohamed
Munampa lawama kocha bila sababu mabeki wenyewe wazembe tu
Sadick
Tatizo la Barcelona sio Kocha pekee yake inahitajika kufanya mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na kurudi kwenye sera yao ya kusajiri wachezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufikiria kuendana na falsafa ya timu kucheza mpira mwingi jambo ambalo wachezaji waliopo hawamudu tena#meridianbettz
Omary lukumbi
Ujue Barcelona wanakua na maamuz ya haraka tatizo sio kocha tatizo ni wachezaj aliokua nao umri mkubwa hakuna replacement yao karibja kikosi kizima kina wa wachezaj wazee
Devotha
Maoni; Mimi ningekua bosi pale ningeipangua Barcelona yote nikaanza upya
Amiri Kayera
Kocha anaajiliwa ili atimuliwe
warda
Watapata timu nyingine tu