Ni usiku wa May 28 2017, muamuzi ametoka tu kupuliza kipenga chake kuumaliza mchezo wa Roma dhidi ya Genoa. Ushindi wa 3-2 wala haujawapa furaha mashabiki wa Roma. Leo shujaa wao Franseco Totti alikuwa anacheza kwa mara ya mwisho.

Totti, Siku ya Mwisho ya Franseco Totti Pale Stadio Olimpico, Meridianbet

Mzee mmoja jukwaani alikuwa na bango limeandikwa ‘Totti lui è maggiore di Roma‘ akimaanisha, baada ya mji wa Roma kwa ukubwa wa historia anafuata Franseco Totti. Heshima ya namna gani ile kufananishwa na mji unaobeba historia ya dunia??

Siku hiyo Screen zote za Stadio Olimpico zilisitisha kuonesha matukio yanayoendelea uwanjani, wakaweka picha maalum ya Totti aliyoipiga ndani ya basi la timu 2001 walipokuwa wametoka kubeba ‘SCUDETTO’. Juu yalikuwepo maneno kadhaa ya kiitaliano ambayo sikuyaelewa.

Totti, Siku ya Mwisho ya Franseco Totti Pale Stadio Olimpico, Meridianbet

Nilimuona bibi mmoja jukwaani akifuta machozi, yeye aliishuhudia safari nzima ya miaka 26 ya Totti ndani ya As Roma. Alikuwa naye kwenye jua kali la saa sita mchana wa Serie A na usiku wa baridi kali sana la usiku wa UEFA. Aliyashuhudia mabao yake 308 na mechi 768 hapa.

Nilimuona mtoto mmoja mdogo wa miaka kama saba hivi, amevaa jezi namba 10 ya Roma. Usoni mwake amejichora jina la Fransesco kwa rangi ya njano. Amepoa kama amemwagiwa maji katikati ya baridi la Njombe.

Camera zilimvuta kwa karibu Rais wa Roma James Pallota, mzee mzima anamwaga machozi ndani ya suti yake ya bei mbaya. Haamini kama yule mtoto aliyekuja hapa na miaka saba tu leo anaondoka. Haamini kama yule Totti aliyekataa kwenda kijiunga na Real Madrid ya Galacticos kwa ajili ya mahaba aliyokuwa nayo kwa Roma leo anaondoka.

Totti, Siku ya Mwisho ya Franseco Totti Pale Stadio Olimpico, Meridianbet

Nilipitia kurasa kadhaa za wachezaji waliokuwa naye safarini. Nilimtazama Gianluigi Buffon akieleza masikitiko yake ya kustaafu kwa Totti. Nilisoma kwa kina maelezo ya Giorgio Chiellini, nilimpitia pacha wake Leonardo Bonucci, wote waliguswa na kuondoka kwa Totti.

Totti, Siku ya Mwisho ya Franseco Totti Pale Stadio Olimpico, Meridianbet

Kumbuka hapa naizungumzia siku ya mwisho ya Fransesco Totti ndani ya Roma.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

Totti, Siku ya Mwisho ya Franseco Totti Pale Stadio Olimpico, Meridianbet

SOMA ZAIDI

16 MAONI

  1. Franseco Totti ni miongini mwa football Legends ambaye hatakumbukwa Daima kwenye soka hasa kwa Timu yake ya Taifa na Roma.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa