Yanga SC imepata pigo kubwa kuelekea mchezo wa debi ya Kariakoo baada ya kubainika wachezaji wawili muhimu kutopatikana kwa mchezo wa Jumamosi.
Yanga Kumkosa Carlinhos na Mustapha Dhidi ya Simba
Yassin Mustapha

Miamba hao wa Jangwani watapambana na wapinzani wao kwa mara ya pili kwenye kampeni hii ya ligi lakini klabu imethibitisha winga Carlos Carlinhos na beki Yassin Mustapha wameondoka kikosini kwa sababu ya majeraha na kwa hivyo watakosa mpambano kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Daktari wa timu ya Yanga Shecky Mngazija amethibitisha wachezaji hao wawili tayari wameruhusiwa kuondoka kambini wanapoanza matibabu ya majeraha yao mbalimbali.

“Carlos Carlinhos atakosa debi kwani tumemwomba akae nje ya uwanja kwa wiki mbili baada ya kupata jeraha,” Mngazija aliiambia maripota.

“Ripoti ya MRI imeonyesha kuwa ana mguu uliovimba na matibabu yake yatachukua muda wa wiki mbili, kwa hivyo hatapatikana kwa mchezo huo.”

Kuhusu Mustapha, Mngizija alisema: “Pia ameonesha kuimarika sana tangu apate jeraha lake lakini hatakuwa tayari kuikabili Simba, hatutaki kumkimbiza kwenye mchezo, tumempa wiki chache arudi akiwa mzima na mwenye nguvu . ”

Hili litakuwa pigo kubwa kwa Yanga na Carlinhos, ambao pia walikosa mchezo wa kwanza kati ya pande hizo mbili mchezo uliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Yanga, Yanga Kumkosa Carlinhos na Mustapha Dhidi ya Simba, Meridianbet

SOMA ZAIDI

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa