Kiongozi wa magoli Laliga na nahodha wa Barcelona, Lionel Messi, anatarajiwa huenda akawa amecheza mchezo wake wa mwisho na Barcelona dhidi ya Celta Vigo.

Ripoti rasmi kutoka Barcelona zinadai kuwa Koeman amemruhusu Messi kutoshiriki mazoezi ya leo na anatarajiwa kukosa mchezo wa Eibar ambapo Barcelona watakuwa wanakamilisha ratiba tu baada ya kujiondoa kwenye mbio za ubingwa.

Mkataba wa Lionel unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, huku kukiwa na fununu kuwa Barcelona watajaribu kumshawishi aongoze mkataba licha ya tetesi kuwa mchezaji huyu anaweza kujiunga na Man City.

Messi amecheza mara 47 katika mashindano yote na Barcelona msimu huu, akifunga magoli 38 na kutoa asisti 11. Naamini kila shabiki wa Barcelona anatamani kuona nguli huyu wa soka akisalia Camp Neo msimu ujao.

UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa