Kocha Mkuu wa klabu ya Coastal Union Juma Mgunda, Amesema kuwa licha ya timu yake kuwa na mwendelezo mbaya wa matokeo ila mapambano yanaendelea ili kuweza kuinasua timu hiyo kwenye janga la kushuka daraja,amesema juma mgunda.

Coastal Union imekuwa na muendelezo mbaya wa matokeo kwani katika mechi 5 zilizopita za timu hiyo kwenye Ligi kuu Tanzania Bara imepoteza michezo 4 na kutoka sare katika mchezo 1.

Coastal Union inasalia katika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 34 katika michezo 31 huku ikisaliwa na michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Simba SC julai 11 kisha Mwadui FC julai 14 na mechi ya mwisho ni dhidi ya Kagera Sugar julai 18.

Mgunda ana kazi ya kukiongoza kikosi cha Coastal Union Kuhakikisha hakishuki daraja huku akiwatakiwa kufanya hivyo katika mechi hizo zilizosalia kabla ya ligi kuu tanzania bara kukamilika.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa