Pengine ni matokeo ambayo wengi hatukuyatarajia kwenye mashindano ya Miami Open 2021. Upande wa wanawake, Naomi Osaka amefungashiwa virago vyake huku Daniil Medvedev akiungana naye kwa upande wa wanaume.

Osaka ambaye ni mchezaji namba 2 kwa ubora duniani, amejikuta akikatishwa safari yake ya kutopoteza michezo 23 mfululizo mikononi mwa Mrusi – Maria Sakkari.

Licha ya Sakkari kupoteza seti ya kwanza kwa matokeo ya 4-1, alionesha ubora wake na kurejea tena mchezoni akimaliza kwa ushindi wa 6-0 6-4. Huu ni ushindi wa 5 mfululizo kwa Sakkari na sasa Naomi Osaka ameyaaga mashindano haya katika hatua ya robo fainali.

Miami Open, Miami Open: Osaka na Medvedev Watolewa Nje., Meridianbet
Sakkari anatua kwenye nusu fainali ya Miami kwa mara ya kwanza.

“Ninafuraha kubwa, ninakosa maneno ya kusema. Kushinda mchezo kama huu, ambao nilikuwa nimezidiwa pointi sita, imenisaidia sana leo. Nimepindua matokeo mara nyingi sana lakini hii inaweza kuwa ni kubwa zaidi.” alisema Sakkari.

Upande wa pili kulikua na mtanange wa Daniil Medvedev dhidi ya Roberto Bautista Agut katika robo fainali ya Miami Open 2021.

Bautista alitumia dakika 92 tu kumuangamiza Medvedev kwa matokeo ya seti 6-4 6-2 na kutinga nusu fainali yake ya 4 kwenye ATP Masters 1000.

Miami Open, Miami Open: Osaka na Medvedev Watolewa Nje., Meridianbet
Medvedev (kushoto) akipongezana na Bautista (kulia) baada ya mchezo wao wa robo fainali.

“Ninataka kumpongeza Daniil. Najua ni miongoni mwa wachezaji bora duniani. Amekuwa akishinda michezo mingi, ni mchezaji wa pili duniani. 

“Nimefurahi na ninajivunia sana kwa nilivyocheza leo. Ninadhani nimeonesha uwezo mkubwa uwanjani.” alisema Bautista.

Kwa matokeo haya, Maria Sakkari atachuana na Bianca Andreescu wakati ambapo Roberto Bautista Agut atapambana na Jannik Sinner kwenye nusu fainali ya Miami Open 2021.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Miami Open, Miami Open: Osaka na Medvedev Watolewa Nje., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa