Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Malaika Mihambo, amelishindia taifa lake medali ya dhahabu katika mashindano ya michezo ya Olimpiki ya long Jump.

 

mihambo, Mihambo : Mtanzania Anayepeperusha Bendera ya Ujerumani Olimpiki., Meridianbet

Mwanaridha huyo aliruka urefu wa mita saba ili kuchukua ushindi. Awali Mihambo alikabiliwa na changamoto kadhaa kabla ya mashindano hayo lakini hatimaye alifanikiwa kuonesha umahiri wake.

Katika fainali ya mchezo huo iliofanyika jana Jumanne, Malaika hakuonesha ishara zozote za kuibuka mshindi.

Urefu wa mita saba alioruka katika jaribio la sita ulimwezesha kuipatia Ujerumani nishani yake ya kwanza ya dhahabu katika mchezo huo tangu Heike Drechsler aliposhinda mwaka 2000.

Nishani ya fedha ilimwendea mshindi mara nne wa mashindano ya dunia na Olimpiki yaliofanyika mjini London Brittney Reese wa Marekani baada ya kuruka mita 6.97 huku Ese Brume wa Nigeria akijinyakulia medali ya shaba na kuiongezea Afrika idadi ya medali katika michezo hiyo.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa