Kumeendelea kuwepo na maandamano ya mashabiki wa klabu ya Arsenal kwa siku za karibuni wakishinikiza mmiliki wa timu hiyo kuondoka. Mikel Arteta ana picha ya tofauti.

Tangu kuibuka kwa sakata la European Super League, mshabiki na baadhi ya wachezaji waliowahi kuitumikia Arsenal, wamemshutumu Stan Kroenke ambaye ni mmiliki wa klabu hiyo kuwa amewakosea kwa kiasi kikubwa kwa kuiingiza timu hiyo kwenye mpango haramu wa ESL (kama ambayo wadau wa soka walivyouita mpango huu).

Baadhi ya mashabiki wameamua kuweka kambi katika uwanja wa Emirate na wengine wakitumia mitandao ya kijamii kupaza sauti zao zinazolenga kushinikiza Kroenke kuondoka klabuni hapo. Mikel Arteta, anaunga mkono juhudi za wamiliki wa Arsenal.

Kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Villareal kesho usiku, Arteta ameamua kuweka wazi kile anachokiamini kuhusu wamiliki wa Arsenal.

Mikel Arteta, Mikel Arteta Awaunga Mkono Wamiliki Arsenal., Meridianbet
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wakiwa nje ya uwanja wa Emirate na bango linaloshinikiza Kroenke kuondoka klabuni hapo.

“Kumekuwa na maneno mengi sana kwa siku kadhaa. Mashabiki wetu walipaza sauti zao kwenye mchezo dhidi ya Everton, lakini sasa hivi tumepata tamko rasmi na lenye uhakika kutoka kwa wamiliki, nadhani hilo limeisha na wameshasema kile walichokisema.

“Siwezi kuzuia maneno na maono ya watu kama hali hii inavyoendelea, ninachopenda kukijua na kukiongelea ni uhalisia. Uhalisia ni kwamba, tunawamiliki ambao wamejipanga kikamilifu na wanataka timu ifanikiwe ndani na nje ya uwanja na wapo tayari kufanya chochote wanachoweza kukifanya ili kufanikisha hilo” alisema Mikel Arteta.

Kroenke alianza kuwekeza Arsenal mwaka 2007 kwa kuwa na hisa ya 9.9%, taratibu aliongeza hisa zake mpaka kufikia 62.89% mnamo mwezi Aprili 2011. 2018, Kroenke alifanikiwa kuinunua Arsenal kutoka kwa Alisher Usmanov kwa dau la pauni milioni 550.

Ukiacha klabu ya Arsenal, Kroenke anamiliki timu ya Los Angeles Rams inayocheza ligi ya NFL nchini Marekani pamoja na timu ya Denver Nuggets inayocheza ligi ya NBA.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa