Mino Raiola Pengine huyu ndiye binadamu anayechukiwa zaidi na Sir Alex Fergie. Si kwasababu alisumbuana nae uwanjani bali namna alivokuwa mafia na mchafu sokoni. Biashara zake zilijaa giza sana.

Mwaka 2012, Paul Pogba akiwa kijana mdogo tu wa miaka 19, Raiola alimfuta na kumuambia, “hawa wote wanaocheza hapa hawana uwezo wako, unajipotezea muda tu. Twende nikupeleke mahali utakapoishtua dunia”

Mino Raiola
Mino Raiola

Kumbuka kwenye kiungo cha Man United kipindi hicho yupo Paul Scholes, Michael Carick, Tom Cleverley, Ryan Gigs na Shinji Kagawa kwa kuwataja wachache tu.

Pogba akahadaika kwa ushawishi wa wakala wake na kukubali kuondoka. Mino alimpeleka Pogba Juventus bure. Lakini Mino alikuwa na mahesabu yake kichwani.

Aliweka kipengele kwenye mkataba wa Pogaba kitakachompatia asilimia 25 ya mauzo kama Juventus watamuuza Pogba kwenda popote pale.

Miaka minne baadae Real Madrid, Man United na Chelsea waligonga mlango kwa Mino Raiola wakitaka huduma ya Pogba. Muda wa Raiola wa kujilipa ukafika.

Aliwaweka kwenye ulingo unaoitwa pesa na kuwataka wapimane uwezo. Man United walishinda na kukubali kuvunja rekodi ya dunia ya usajili. Mino Raiola akachukua paundi milioni 22 na kutokomea zake. ‘Mind you’ hii pesa aliyolipwa ingeweza kumsajili Mario Gotze kwa kipindi kile.

Hizi biashara nyeusi alizianza zamani kwa akina Frank Rijkaard na Denis Berkgamp. Hii michezo michafu sokoni ndiyo chakula chake. Unakumbuka 2010 alivowazunguka Chelsea na kumpeleka Robinho Man City? Huyu ndiyo Mino Raiola halisi na sura ya pesa.

Wakati huu kila mtu akimmezea mate Erling Haaland, yeye amechimbia zake Monaco na simu yake ya mkononi. Anachobadilisha ni mataifa tu anayopiga. Bahati mbaya siri zake haziwezi kuvuja kwasababu hana hata mkalimani. Anazungumza lugha nane peke yake.
Mino Raiola
Mino Raiola

Ameshasema zipo timu 10 tu duniani zinazoweza kumsajili Erling Haaland kwa sasa, nne kati ya hizo zipo ligi kuu ya Uingereza. Unazijua ni zipi??

Hakuna anayejua, hata yeye labda hazijui. Kinachojulikana ni kuwa Erling Haaland atapandisha tarakimu za pesa katika akaunti yake ya benki. Atapandishaje?? Ni suala la kusubiri muda na kuiona sura halisi ya Mino Raiola. Sura ya pesa.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Mino Raiola, Mino Raiola na Mitego ya  Pesa Nyingi kwa Wachezaji wake, MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa