Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Italia, timu hizi zipo kwenye sandakalawe, zote mbili zinajiandaa kufanya dili la mabadilishano na nyota Moise Kean ambaye hana uhakika na hatma yake PSG.

Kean aliungana na miamba hawa wa Ligue 1 kwa mkopo akitokea Everton oktoba iliyopita, lakini nyota huyu alikiri kuwa bado hana uhakika kuwa ataichezea klabu gani msimu ujao.

kwa mujibu wa Tuttosport, wote wawili, Juventus na Inter wamemuweka nyota huyu kuwa kipaumbele kuelekea msimu wa ujao 2021-22.

Mipango ya Juventus na Inter kwa Kean
Kean ni zao akademi ya soka ya Juventus

Taarifa zinasema kuwa Inter Milan wao wanajiandaa kufanya dili la mabadilishano na Everton ambalo litamhusisha Matias Vecino na malipo ya ziada ya fedha.

Wakati huo Juventus wao wakiripotiwa kuwa wapo tayari kumuondoa Merih Demiral kwa ajili ya Kean, na wanatajwa kuwa wanampa kipaumbele staa huyu zaidi ya Sergio Aguero ambaye anatarajia kuondoka Man City baada ya kumaliza mkataba wake.

Kean ni zao la shule ya soka ya Juventus, na alikamilisha uhamisho wake kuelekea Everton mwaka 2019 kwa €30m. Amefunga magoli 18 kwenye mechi 37 za michuanbo yote akiwa na PSG msimu huu.


 

JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

Kean, Mipango ya Juventus na Inter kwa Kean, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa