Mkongwe wa Juventus Giampiero Boniperti amefariki akiwa na umri wa miaka 92 The Bianconeri wamemtangaza siku ya Ijumaa.

Mkongwe wa Juve Boniperti Afariki Akiwa na Miaka 92

Boniperti aliiwakilisha Juve kwa takribani miaka 15 kama mchezaji, akifanikiwa kushinda mataji matano ya Scudetto kati ya mwaka 1946 na 1961.

Alistaafu akiwa amefunga mabao 179kwa klabu hiyo ya Turin, rekodi ambayo ilidumu kwa takribani miaka 40 kabla ya Alessandro Del Piero kuivunja.

Boniperti alicheza mechi 443 pia aliweka alama kwa Juventus ambayo ilipitwa na Del Piero.

Gwiji huyo wa klabu alikuwa rais wa Juventus mwaka 1971, na kushuhudia klabu ikishinda mataji 16 na baadaye alipewa taji la heshima.

Mkongwe wa Juve Boniperti Afariki Akiwa na Miaka 92
Giampiero Boniperti, mwaka  1961. 

“Ushindi siyo kitu cha umuhimu, lakini ndiyo kitu kinachotakiwa,” ilikuwa nukuu yake maarufu.

“Leo Juni 18 2021, tunatoa pole zetu kwa Giampiero Boniperti, ambaye amfariki akiwa na umri wa miaka 92 huko Turin” ilikuwa ni taarifa kutoka katika klabu ya Juventus.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa