James Rodríguez Ajiunga na Colombia kwa Maandalizi ya Kombe la Dunia

Kiungo wa zamani wa Real Madrid, James Rodríguez ameondoka kwa hisia mseto kuelekea kambi ya timu ya taifa ya Colombia baada ya klabu yake ya MLS, Minnesota United FC kupokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Colorado Rapids katika mechi iliyochezwa Jumanne usiku.

James Rodríguez Ajiunga na Colombia kwa Maandalizi ya Kombe la DuniaMinnesota United ilipoteza mchezo huo wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS), matokeo ambayo yalikuwa ya kukatisha tamaa kwa James kabla ya kuungana na timu ya taifa kwa maandalizi ya Kombe la Dunia.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kabla ya mchezo huo, klabu ya Minnesota United ilithibitisha kuwa kiungo huyo ataruhusiwa kujiunga na kambi ya Colombia, huku zikiwa zimebaki mechi mbili kabla ya ligi kusimama kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia.

James Rodríguez Ajiunga na Colombia kwa Maandalizi ya Kombe la DuniaKatika taarifa yao, klabu hiyo ilisema “Klabu inajivunia kumsaidia James akiwa anaiwakilisha nchi yake kwenye jukwaa kubwa zaidi duniani na inamtakia mafanikio katika kambi na mashindano yote,” ilisema taarifa hiyo.

James Rodríguez Ajiunga na Colombia kwa Maandalizi ya Kombe la DuniaRodríguez alijiunga na Minnesota United kama mchezaji huru mwezi Februari, akiwa na mkataba unaotarajiwa kumalizika Juni wakati wa kipindi cha Kombe la Dunia, huku klabu ikiwa na chaguo la kuongeza mkataba hadi mwisho wa mwaka, ingawa dalili zinaonyesha haitalichukua.

James Rodríguez Ajiunga na Colombia kwa Maandalizi ya Kombe la DuniaKatika mechi sita alizocheza MLS, zikiwemo mbili alizoanza kama kikosi cha kwanza, James amefanikiwa kutoa pasi mbili za mabao bila kufunga bao lolote. Akizungumza kwa ufupi baada ya mchezo, alisema “Ni wakati muhimu kwangu kwenda kuitumikia nchi yangu. Nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ninarudi nikiwa na nguvu zaidi kwa Colombia.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.