Nahodha wa Argentina, Lionel Messi ameonyesha kiwango cha juu baada ya kufunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili, akiiongoza Inter Miami CF kushinda 5-3 dhidi ya FC Cincinnati katika mchezo wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS) uliochezwa ugenini.
Kwa matokeo hayo, Inter Miami imeendelea kuimarika msimamo wake katika Kanda ya Mashariki ikiwa na pointi 25, huku Messi akiendelea kuwa katika kiwango bora kabla ya Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika Amerika ya Kaskazini.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Messi alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 24 baada ya kufuatilia mpira uliotokana na makosa ya beki Matt Miazga, kisha Cincinnati kusawazisha kupitia penalti ya Kevin Denkey dakika ya 41, na kwenda mapumziko sare ya 1-1.
Baada ya mapumziko, Cincinnati walitangulia tena kupitia Pavel Bucha, lakini Messi alirejesha matumaini ya Inter Miami kwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya 55 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akimalizia pasi ya Rodrigo De Paul.
Cincinnati waliendelea kupambana na kurejea mbele kupitia Evander dakika ya 64, lakini Inter Miami walipata mabao mengine kupitia Mateo Silvetti pamoja na mchezaji wa Mexico German Berterame kabla ya Messi kuhusika tena kwenye bao la mwisho dakika ya 89, ambapo shuti lake liligonga mwamba na kumgonga kipa Roman Celentano na kuwa bao la kujifunga.
Kocha wa Inter Miami, Guillermo Hoyos, aliisifu timu yake akisema “Walichofanya leo kilikuwa cha kuvutia dhidi ya timu ngumu na kwenye uwanja mgumu. Ni vigumu sana kucheza hapa.”
Aliongeza “Ni wazi kwamba hawapo MLS kwa matembezi tu. Wapo hapa kucheza, kutoa kila kitu, na kuonyesha dunia kwamba soka linachezwa hapa pia. Tunaondoka tukiwa na furaha kubwa. Tulicheza kiwango cha juu sana cha soka.”


