Inter Miami CF hatimaye wamepata ushindi wao wa kwanza katika uwanja wao mpya baada ya kuichapa Portland Timbers mabao 2-0 katika mchezo wa Major League Soccer (MLS).

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufunga bao moja na kutoa assist ya kuvutia iliyowasaidia mabingwa hao watetezi wa MLS kuibuka na ushindi muhimu mbele ya mashabiki wao.
Messi alianza kuonyesha makali yake dakika ya 30 baada ya kuanzisha na kumalizia vizuri shambulizi safi lililohusisha Luis Suarez pamoja na Telasco Segovia. Segovia alitoa pasi ya kisigino iliyomkuta Messi ambaye hakufanya kosa kuupachika mpira wavuni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Dakika 10 baadaye, Rodrigo De Paul alifanya kazi kubwa upande wa kulia kabla ya kumpa Messi mpira. Nyota huyo mwenye Ballon d’Or nane aliwapita mabeki kadhaa kwa ustadi mkubwa na kutoa pasi iliyomwezesha German Berterame kufunga bao la pili kwa urahisi.
Kipindi cha pili hakikuwa na mabao licha ya kuendelea kutengeneza nafasi kadhaa. Alikaribia kuongeza bao kwa shuti la mbali lililopita karibu na lango pamoja na mpira wa adhabu wa dakika za majeruhi uliookolewa kwa ustadi na kipa James Pantemis.
“Messi ameonyesha bado ana uwezo mkubwa wa kubadili mchezo muda wowote. Ushindi huu ni muhimu sana kwa timu na mashabiki wetu,” ilielezwa kutoka kambi ya Inter Miami baada ya mchezo huo.
Ushindi huo unaifanya Inter Miami kupanda kileleni mwa Eastern Conference kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Nashville SC, huku Lionel Messi akiendelea kujiandaa kwa Kombe la Dunia litakaloanza mwezi ujao nchini Marekani, Mexico na Canada.


