Mchezaji wa Chelsea, Mason Mount amechaguliwa mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwaka 2020/2021, huku akionesha mchezo mzuri sana kwenye klabu yake na kwenye timu yake ya taifa kote ndani na nje ya michuano ya ulaya.

Kijana huyu mdogo mwenye wa umri wa miaka 22, ameonesha makali yote licha ya mabadiliko ya walimu ambayo yametokea pale Stamford Bridge. Akiwa chini ya Frank Lampard, Mount alikuwa wa moto sana katika eneo la katikati, kushambulia licha ya kujali atatokea kati au pembeni.

Mount amekuwa mwiba wa moto kwa wapinzani pindi anapokuwa uwanjani na amesaidia timu yake ya Chelsea kufanya makubwa sana msimu na mpaka sasa kuwa kwenye fainali ya Kombe la ligi ya mabingwa ulaya ambayo itapigwa mwishoni mwa mwezi huu dhidi ya mabingwa wa EPL, Manchester City.

mOUNT
mOuNT amecheza dakika nyingi zaidi ya mchezaji yoyote wa Chelsea
Mount anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutokea kwenye akademi ya timu hiyo toka tukio hilo lifanywe na John Terry mwaka 2006.

Huu waweza kuwa mwanzo mzuri kwa kinda huyu ambaye anaonekana kuja kwa kasi sana chini ya Tuchel ambaye ameibadili Chelsea kwa kiwango kikubwa sana toka ujio wake pale Darajani. Akiwa na Chelsea msimu huu amecheza mechi 34 na kufunga magoli 6 huku akitoa pasi za magoli 6 pia, ila anapokuwa uwanjani basi huwa anawaonea sana wapinzani.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

mount, Mount Awa Mchezaji Bora Wa Chelsea 2020/2021, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa