Mourinho ameendelea na jitihada zake za kutengeneza kikosi cha Roma toka achaguliwe na kutangazwa kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho.

Jose ameamua kukisuka upya kikosi cha Roma kwa lengo la kuhakikisha wanapambania mataji msimu ujao. Jose anarejea Serie A baada ya miaka mingi ya kuhangaika nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza.

Kipenzi cha kocha huyo, Nemanja Matic, ni miongoni mwa tageti ambazo zinahitajika kuboresha kikosi cha Roma kwa msimu ujao.

Matic anaweza kuwa sokoni msimu ujao kwa dau la euro milioni 7 tu mwisho wa msimu huu, kwa kinachosadikika kuwa ni kupunguza gharama. Mchezaji huyo wa Kiserbia alijiunga na Chelsea mwaka 2014 kwa dau la Euro milioni 21, na baada tena kujiunga na United mwaka 2017 kwa euro milioni 40.

Morinho ataman matic1
Matic akiwa mchezaji wa Chelsea enzi za Mourinho
Hii inaweza kuwa ni mara ya tatu kwa Mourinho kumfundisha Matic na mara zote wamekuwa wakishirikiana kuchukua makombe huko kote walipopita pamoja.
Mourinho amtaka Matic Roma
Matic akipeana mkono na Mourinho kipindi cha Mourinho akiwa United

Roma wamedai kukubali chochote kile kitakachosaidia klabu hiyo, na endapo tu Jose ataeleza kuwa Matic ni chaguo lake kuu basi atasajiliwa licha ya kuwa na mkataba na United mpaka 2023.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa