Timu ya AS Roma ya Italia imemtangaza Jose Mourinho kuwa Kocha wake ikiwa ni wiki mbili tangu kibarua chake kiote nyasi akiwa Tottenham Hotspurs, aliyodumu nayo kwa muda wa miezi 17.

Mourinho mwenye umri wa miaka 58 ambaye ni raia wa Ureno, amesaini kandarasi ya miaka mitatu na ataanza kuinoa AS Roma mwanzoni mwa msimu ujao.

Mourinho-RomaKocha huyo aliyewahi kufundisha Klabu za Porto, Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Manchester United, akiwa Tottenham alishinda michezo 45, kufungwa 24 na kutoka sare 17.

Baada ya mambo kuwa magumu ndani ya Ligi Kuu England anarejea ndani ya Serie A ambapo huko alifanya kazi kwa mafanikio alipokuwa huko.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

mourinho, Mourinho Atua AS Roma Rasmi, Meridianbet

SOMA ZAIDI

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa