Klabu ya Azam imemtambulisha rasmi nahodha wa zamani wa timu ya Gor Mahia ya Kenya Kenneth Muguna kwa dili la miaka miwili kuelekea msimu ujao.

Azam imeendelea kuimarisha kikosi chake na inaonekana wamepania kufanya makubwa msimu ujao baada ya kuwa wasindikizaji wa VPL kwa muda sasa.

Muguna anajiunga na Azam akitokea Kenya ambapo aliaga jumanne iliyopita akidai kwenda kutafuta changamoto nyingine bila kutaja atafikiwa wapi.

Mchezaji huyo wa Kenya anaenda kujiunga na wanalambalamba akiwa kama kiungo mshambuliajia ambaye anajiunga na wenzake watatu ambao wameshasajiliwa akiwemo Charles Zulu, Rodgers Kola na Edward Manyama.

Muguna ni miongoni mwa nyota wanaotamba kwenye soka la Kenya, msimu huu akifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la FA la nchini huko, huku timu yake ya Gor Mahia ikiibuka mabingwa wa michuano hiyo.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa