Kocha wa Ujerumani, Joachim Low amewarudisha kikosini wakongwe, Thomas Muller na Mats Hummels baada ya kuondolewa katika kikosi hicho kwa takribani miaka miwili iliyopita.

Muller na Hummels wametajwa katika kikosi cha wachezaji 26 wa kikosi cha Ujerumani kilichoitwa kwaajili ya mashindano ya Euro 2020 yanayotarajiwa kuanza June 11.

Wachezaji hao waliondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 2019 wakati meneja Joachim Low alipokuwa anataka kuweka vijana katika timu hiyo.

Hummels ambaye alicheza na Muller pale Bayern Munich kati ya mwaka 2016 na 2019 aliweka wazi furaha yake katika akaunti yake ya twitter iliyosomeka ” Ninafuraha kuichezea tena timu yangu ya taifa ya Ujerumani”.

Muller pia aliweka ujumbe wake ulioambatana na picha yake uliosomeka ” Nimerudi tena timu ya DFB”.

Wachezaji hao walikuwa katika kikosi cha Low kilichochukua kombe la dunia mwaka 2014.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

muller, Muller, Hummels Warudi Kikosini Euro 2020., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa