Thomas Muller amekiri kwamba yupo tayari kufuata nyayo za Thiago Alcantara kwa kuondoka huko Allianz Arena na kusisitiza “sijazuiwa” na Bayern Munich.
Muller Mbioni Kufuata Nyayo za Thiago Alcantara
Thomas Muller

Muller alianza kucheza soka la kulipwa huko Bayern Munich mwaka 2008 na tangu kipindi hicho ameisadia klabu kupata mafaniko makubwa ndani ya Ujerumani na katika Ligi ya Mabingwa.

Mchezaji huyo wa miaka 31 bado amesalia kuwa ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi lakini ni kama anaonekana kukaribia kufanya maamuzi kama Thiago alivyohamia Liverpool mwaka 2020na kudhihirisha kwamba hakuna mtu ambaye hawezi kuondoka klabuni.

“Sijafungwa katika klabu hii,” Fowadi huyo wa Bayern aliiambia Times. “Nina uhusiano maalumu, Ninaipenda Bayern Munich kabla hata sijaanza kuichezea lakini kama kuna hali inayokupelekea kufanya maamuzi labda ya kwenda klabu nyngine unafanya na haitakuwa aibu wala haitakuwa tatizo.

Muller amecheza michezo 571 katika mashindano yote kwa Bayern Munich na amefanikiwa kufunga mabao 212 na kutoa assist 210. Mshambuliaji huyo amefanikiwa kushinda mataji 27 makubwa, Tisa ya Bundesliga na mawili ya Champions League.

Mkataba wa sasa wa Muller unatarajiwa kumalizika mwaka 2023 na Hansi Flick amekuwa akimuamini sana katika kuongoz kikosi akisadiana na Lewandowski.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Muller, Muller Mbioni Kufuata Nyayo za Thiago Alcantara, Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa