Kocha wa Yanga SC, Nasreddine Nabi ameelezea wasiwasi wake kwenye kikosi chake, akisisitiza lazima waimarike kwa mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara.

Nabi Apata Wasiwasi Juu ya Safu ya Ushambuliaji ya Yanga

Kwa mujibu wa kocha huyo wa Tunisia, ambaye bado hajashinda mechi kwenye ligi kuu tangu achukue nafasi ya Cedric Kaze, wababe hao wa Jangwani wanatengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini washambuliaji hawazitumii.

Nabi amewambia maripota atashughulikia hali hiyo na atahakikisha washambuliaji wake wanaanza kuipata mabao yanga, kwenye mchezo ujao wa ligi dhidi ya JKT Tanzania mjini Dodoma Jumatano.

“Ni kitu ambacho kinanitia wasiwasi sana, na sina furaha juu yake, tunaunda nafasi kadhaa lakini washambuliaji wangu hawafungi mabao,” Nabi aliiambia maripota.

“Nitaendelea kufanya kazi kwenye eneo hilo, nataka kuhakikisha mshambuliaji wangu anaweza kufunga mabao, nitakuwa na raha tu nitakapowaona washambuliaji wangu wakifunga mabao, ni jambo ambalo ninafanya kazi na benchi langu la ufundi, kwa sababu bila magoli, basi haushindi chochote.

Kwa sasa Yanga wanaunyatia ubingwa na watahitaji kuipiga JKT ili kupunguza pengo kati yao na wapinzani wao Simba SC, ambao wako kileleni mwa jedwali.

Dhidi ya JKT, Yanga itakuwa ikiangalia kupata ushindi mwingine baada ya kushinda mchezo wa raundi ya kwanza kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Nabi, Nabi Apata Wasiwasi Juu ya Safu ya Ushambuliaji ya Yanga, MeridianbetBASHIRI SASA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa