Mshambuliaji wa zamani wa Argentina, Gabriel Batistuta, ameibua mjadala mpya baada ya kumchagua Diego Maradona kama mchezaji bora zaidi kwake kumzidi Lionel Messi, akisisitiza tofauti ya haiba na uwezo wa uongozi kati ya nyota hao wawili.
Batistuta, ambaye alipata nafasi ya kucheza sambamba na Maradona katika timu ya taifa ya Argentina, amesema kuwa alishuhudia moja kwa moja uwezo wa kipekee wa mkongwe huyo ndani na nje ya uwanja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kuhusu ubora wa Maradona, Batistuta alisema, “Maradona alikuwa na uwezo wa kucheza, kuongoza timu, na kushughulikia waamuzi na wapinzani. Alikuwa na uwezo wa kufanya mambo ya ajabu.” Kauli hiyo inaonyesha namna anavyothamini mchango wa gwiji huyo katika soka.
Ameongeza kuwa tofauti kubwa ipo katika haiba ya uongozi, akieleza kuwa Maradona alikuwa na ushawishi mkubwa kwa wachezaji wenzake na aliweza kubeba timu katika nyakati ngumu.
Kwa upande wa Messi, Batistuta hakupunguza uwezo wake wa kiuchezaji, lakini alisisitiza kuwa kuna mambo ya ziada ambayo Maradona alikuwa nayo na ni vigumu kufikiwa.

