Mabingwa wa dunia mara tano, timu ya taifa ya Brazil wamewasili rasmi jijini Orlando kuanza maandalizi ya mechi zao za kirafiki za kimataifa zitakazopigwa nchini Marekani.
Kikosi hicho kimeweka kambi Orlando kikijiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya France utakaochezwa Alhamisi, Machi 26, 2026 majira ya saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Gillette Stadium.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Baada ya hapo, Brazil itashuka dimbani tena kuikabili timu ya taifa Croatia katika mchezo wa pili wa kirafiki utakaopigwa Jumatano, Aprili 1, 2026 saa 09:00 alfajiri.
Nyota wakubwa wa kikosi hicho akiwemo Vinícius Júnior na Rodrygo wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji, wakisaidiwa na kundi zima la wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.
Mashabiki wa soka jijini Orlando wanatarajiwa kushuhudia burudani ya hali ya juu kutoka kwa mastaa wa Brazil wanaocheza soka la kuvutia la “Joga Bonito”, huku timu hiyo ikilenga kujiimarisha zaidi kabla ya majukumu makubwa yajayo ya kimataifa.


