Broos Aona Matumaini Licha ya Kipigo cha Mexico, Alaumu Kadi Nyekundu

Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos, amesema bado ana matumaini ya timu yake kufanya vizuri katika mashindano makubwa Duniani 2026 licha ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Mexico katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A uliochezwa kwenye Estadio Azteca.

Broos Aona Matumaini Licha ya Kipigo cha Mexico, Alaumu Kadi NyekunduMabao ya Julian Quinones na Raul Jimenez yaliipa Mexico ushindi mbele ya mashabiki zaidi ya 80,000, lakini Broos alisisitiza kuwa matokeo hayo hayaakisi namna ambavyo Afrika Kusini ilijipanga vizuri katika safu ya ulinzi kwa sehemu kubwa ya mchezo huo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Unacheza michuano dhidi ya timu bora, lakini tulicheza vizuri. Niliona Mexico iliyokuwa na presha kubwa na mara nyingi hawakujua wafanye nini na mpira. Mpangilio wetu wa ulinzi ulikuwa mzuri sana,” alisema Broos akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo.

Broos Aona Matumaini Licha ya Kipigo cha Mexico, Alaumu Kadi NyekunduHata hivyo, kocha huyo alikiri kuwa timu yake ilikosa ubunifu na makali katika eneo la ushambuliaji, jambo ambalo linafaa kufanyiwa kazi kabla ya mechi zijazo. “Kwenye upande wa ushambuliaji tunapaswa kuboresha zaidi. Tukicheza kwa kiwango kilekile cha ulinzi lakini tukawa bora zaidi mbele ya lango, nina uhakika tutapata matokeo mazuri,” aliongeza.

Broos Aona Matumaini Licha ya Kipigo cha Mexico, Alaumu Kadi NyekunduChangamoto kubwa kwa Afrika Kusini imekuwa kadi nyekundu mbili walizozipata Sphephelo Sithole na Themba Zwane, huku nahodha wa Mexico Cesar Montes naye akitolewa nje kwa kadi nyekundu. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa wamichuano mikubwa kushuhudia kadi nyekundu tatu. Broos alisema anakubaliana na kadi ya Sithole lakini ana mashaka kuhusu ile ya Zwane. “Kadi ya kwanza tunaweza kuikubali, lakini ya pili inaweza kujadiliwa kwa sababu mchezaji wa Mexico ndiye aliyemzuia mchezaji wangu. Hata hivyo, huo ni uamuzi wa mwamuzi na tunapaswa kuukubali,” alisema.

Broos Aona Matumaini Licha ya Kipigo cha Mexico, Alaumu Kadi NyekunduLicha ya kuwakosa Sithole na Zwane katika mchezo ujao dhidi ya Czech Republic mjini Atlanta, Broos anaamini timu yake bado ina uwezo wa kurejea kwenye mstari wa ushindi. “Tunahitaji siku chache kuondoa maumivu ya matokeo haya na uchovu wa mchezo. Baada ya hapo tutafanyia kazi ushambuliaji wetu kwa sababu leo haukuwa wa kutosha. Tukionyesha ari na nidhamu kama tulivyofanya leo, nina uhakika tutapata matokeo mazuri katika mechi mbili zilizobaki,” alisema kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.