Kikosi cha timu ya taifa ya England kimeondoka leo kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026, huku kikibeba matumaini makubwa ya kuwania taji hilo chini ya uongozi wa kocha mkuu Thomas Tuchel.
Simba hao watatu wanatarajiwa kuweka kambi yao katika mji wa Kansas City, wakitumia kituo cha mazoezi cha Swope Soccer Village kama sehemu ya maandalizi yao ya mwisho kabla ya kuanza rasmi kampeni ya michuano hiyo mikubwa duniani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“England imeondoka kuelekea Marekani ikiwa na malengo makubwa ya kufanya vizuri na kuwania ubingwa wa dunia chini ya kocha Thomas Tuchel,” zimeeleza taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho.
Katika kipindi cha maandalizi, England itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya New Zealand na Costa Rica, michezo ambayo itatumika kupima utayari wa kikosi kabla ya kuanza kwa mashindano rasmi.
“England imepangwa Kundi L na itaanza safari yake ya kusaka ubingwa wa Kombe la Dunia kwa kucheza dhidi ya Croatia Juni 17.” Mashabiki wa taifa hilo wana matumaini kuwa kizazi cha sasa cha wachezaji kitaweza kurejesha heshima ya England kwenye jukwaa kubwa la soka duniani.


