Timu ya taifa ya Misri imelazimika kufanya mabadiliko ya ghafla kwenye jezi zake za michuano mikubwa ya Dunia 2026 baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA kuagiza kuondolewa kwa nyota saba zilizokuwa zimewekwa juu ya nembo ya taifa hilo.
Nyota hizo zilikuwa zikionyesha mafanikio ya Misri katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ambapo imewahi kutwaa taji hilo mara saba. Hata hivyo, FIFA imeeleza kuwa kwa mujibu wa kanuni zake, nyota zinazowekwa kwenye jezi za timu za taifa zinapaswa kuwakilisha mataji ya Kombe la Dunia pekee. “Matumizi ya nyota kwenye jezi za Kombe la Dunia yanapaswa kuhusishwa na ubingwa wa mashindano hayo pekee,” imeeleza FIFA.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mbali na suala la nyota hizo, FIFA pia ilielekeza kufanyika kwa marekebisho kwenye majina na namba za wachezaji zilizokuwa zimeandikwa kwa rangi ya dhahabu. Shirikisho hilo lilisema maandishi hayo hayakuwa yanaonekana vizuri katika matangazo ya televisheni, jambo ambalo lingeweza kuathiri ufuatiliaji wa mechi kwa watazamaji duniani.
Kutokana na maelekezo hayo, maandishi ya dhahabu yameondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na rangi nyeupe ili kuboresha mwonekano wa jezi hizo. “Mabadiliko hayo yanalenga kuhakikisha viwango vya mwonekano na utambulisho wa wachezaji vinazingatiwa katika matangazo ya televisheni,” imefafanuliwa katika taarifa ya mashindano.
Kampuni ya Puma, inayosimamia utengenezaji wa jezi za Misri, imelazimika kufanya marekebisho hayo kwa haraka kabla ya mchezo wa kwanza wa Kundi G. Misri inatarajiwa kushuka dimbani Juni 15, 2026 kuikabili Ubelgiji katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani.


