Goli la McTominay Lawekwa Kwenye Noti Baada ya Scotland Kurejea Kombe la Dunia

Kiungo wa timu ya taifa ya Scotland Scott McTominay amepewa heshima ya kipekee baada ya bao lake la kuvutia dhidi ya Denmark kuwekwa kwenye noti maalum ya pauni 20 iliyozinduliwa na Bank of Scotland kwa ajili ya kuadhimisha kurejea kwa Scotland katika Fainali za Kombe la Dunia baada ya miaka 28.

Goli la McTominay Lawekwa Kwenye Noti Baada ya Scotland Kurejea Kombe la DuniaMcTominay aliingia kwenye historia ya soka la Scotland baada ya kufunga bao la kubinuka (overhead kick) katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Denmark kwenye mchezo wa mwisho wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 uliochezwa Novemba 18, 2025. Bao hilo lilifungwa katika dakika ya pili ya mchezo na kusaidia Scotland kuongoza Kundi C pamoja na kufuzu rasmi kwa michuano hiyo itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa Benki ya Scotland, noti hizo maalum ni 100 pekee zilizochapishwa, huku 50 kati yake zikitarajiwa kupatikana kupitia mnada wa wakusanyaji, droo za zawadi pamoja na “vaults” maalum zitakazowekwa katika miji ya Glasgow na Edinburgh.

Goli la McTominay Lawekwa Kwenye Noti Baada ya Scotland Kurejea Kombe la Dunia“Bao lile limekuwa sehemu ya historia ya taifa letu na lilistahili kuenziwa kwa njia ya kipekee,” ilieleza taarifa ya Benki ya Scotland wakati wa uzinduzi wa noti hizo maalum zinazomuenzi McTominay kwa mchango wake mkubwa kwa taifa hilo.

Goli la McTominay Lawekwa Kwenye Noti Baada ya Scotland Kurejea Kombe la DuniaAidha, sehemu ya mapato yatakayopatikana kutokana na noti hizo maalum yataelekezwa kwa Crisis Scotland, taasisi inayosaidia watu wasio na makazi nchini Scotland, huku mashabiki wengi wakielezea hatua hiyo kama kumbukumbu muhimu ya mafanikio ya timu yao ya taifa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.