Guardiola Aripotiwa Kuzungumza na Maldini Kuhusu Kuinoa Timu ya Taifa ya Italia

Kocha wa zamani wa Manchester City, Pep Guardiola, ameripotiwa kufanya mazungumzo na mkurugenzi mpya wa ufundi wa Shirikisho la Soka Italia (FIGC), Paolo Maldini, kuhusu uwezekano wa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Italia. Kwa mujibu wa wa taarifa za nchini Italia, wawili hao walikutana jijini Barcelona mwishoni mwa wiki iliyopita kujadili mustakabali wa timu hiyo maarufu kama Azzurri.

Guardiola Aripotiwa Kuzungumza na Maldini Kuhusu Kuinoa Timu ya Taifa ya ItaliaTaarifa zinaeleza kuwa Maldini aliambatana na mshauri wake Leonardo katika safari hiyo, ambapo lengo kuu lilikuwa kupima utayari wa Guardiola kuongoza mradi mpya wa kuijenga upya Italia. Mazungumzo hayo yamezidisha uvumi kwamba kocha huyo wa Hispania anaweza kuwa mmoja wa wagombea wakuu wa nafasi hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Kuna majina mengine pia yanayozingatiwa,” alisema Rais wa FIGC, Giovanni Malagò, akifafanua kuwa mchakato wa kumteua kocha mpya haujahitimishwa. Aliongeza kuwa pamoja na Guardiola, majina ya Roberto Mancini na Andrea Pirlo pia yanaendelea kutajwa katika orodha ya wanaowania nafasi hiyo.

Guardiola Aripotiwa Kuzungumza na Maldini Kuhusu Kuinoa Timu ya Taifa ya ItaliaMalagò alisisitiza kuwa uamuzi wa mwisho hautategemea tu utayari wa makocha wanaotajwa, bali pia uwezo wa kifedha wa shirikisho hilo kulingana na bajeti ya mwaka 2026. “Ni lazima uchaguzi wa kocha mpya uendane na uwezo wa kifedha wa FIGC,” alieleza.

Guardiola Aripotiwa Kuzungumza na Maldini Kuhusu Kuinoa Timu ya Taifa ya ItaliaHadi sasa, FIGC haijatoa tamko rasmi kuhusu nani atakayeteuliwa kuiongoza Italia, lakini jina la Pep Guardiola linaendelea kuvuta hisia huku mashabiki na wadau wa soka wakisubiri kwa hamu uamuzi wa mwisho kuhusu benchi la ufundi la mabingwa hao wa zamani wa dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.