Hong Myung-bo Aisifu Korea Kusini kwa Umoja Baada ya Ushindi dhidi ya Czech Republic

Kocha wa timu ya taifa ya Korea Kusini, Hong Myung-bo, amepongeza ari ya umoja na mapambano ya wachezaji wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Czech Republic katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi A la michuano mikubwa ngazi ya Dunia 2026 uliochezwa Alhamisi mjini Guadalajara.

Hong Myung-bo Aisifu Korea Kusini kwa Umoja Baada ya Ushindi dhidi ya Czech RepublicKorea Kusini ilijikuta nyuma katika kipindi cha pili baada ya beki Ladislav Krejci kuifungia Czech Republic bao la kuongoza kwa kichwa. Hata hivyo, Wakorea walionyesha moyo wa kupambana na kufanikiwa kurejea mchezoni kupitia mabao ya Hwang In-beom na Oh Hyeon-gyu na kujihakikishia pointi tatu muhimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo huo, Hong alisema wachezaji wake walitekeleza kikamilifu maelekezo aliyowapa kabla ya mechi. “Kabla ya mchezo niliwapa ujumbe mbili; kutokukata tamaa hadi mwisho na kubaki wamoja. Iwe uwanjani au nje ya uwanja, tunapaswa kucheza kama timu moja,” alisema kocha huyo.

Hong Myung-bo Aisifu Korea Kusini kwa Umoja Baada ya Ushindi dhidi ya Czech RepublicUshindi huo ulipatikana licha ya nahodha wa timu hiyo, Son Heung-min, kuwa na siku ngumu ambapo alikosa nafasi tano za wazi katika kipindi cha kwanza kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Oh Hyeon-gyu ambaye baadaye alifunga bao la ushindi.

Hong Myung-bo Aisifu Korea Kusini kwa Umoja Baada ya Ushindi dhidi ya Czech RepublicHata hivyo, Hong alimkingia kifua nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur, akisisitiza kuwa mchango wake ndani ya timu bado ni mkubwa. “Son ndiye mchezaji wetu bora na pia ni nahodha mwenye utulivu mkubwa. Tunaamini alifanya kila alichoweza kwa uwezo wake,” alisema.

Hong Myung-bo Aisifu Korea Kusini kwa Umoja Baada ya Ushindi dhidi ya Czech RepublicKocha huyo alikiri kuwa timu yake inahitaji kuboresha umaliziaji wa nafasi za mabao, huku akielekeza macho kwenye mchezo ujao dhidi ya Mexico Juni 18. Korea Kusini na Mexico zote zina pointi tatu kileleni mwa kundi hilo, jambo linalofanya pambano hilo kuwa na umuhimu mkubwa katika mbio za kufuzu hatua inayofuata ya mashindano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.