Nahodha wa Poland, Robert Lewandowski, amegusa hisia za mashabiki wa soka duniani baada ya tukio lake la kusikitisha kufuatia mchezo dhidi ya Sweden uliomalizika kwa Poland kupoteza kwa mabao 3-2 na kushindwa kufuzu Kombe la Dunia mwaka huu.
Mara baada ya filimbi ya mwisho, Lewandowski alibaki uwanjani kwa muda akionekana kuwaaga mashabiki wa Poland kwa namna ya hisia kubwa, tukio lililozua tafsiri nyingi miongoni mwa wadau wa soka kuhusu hatma yake ndani ya timu ya taifa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Dakika chache baadaye, mshambuliaji huyo wa klabu ya Barcelona alichapisha picha kupitia akaunti yake ya Instagram akiambatanisha na wimbo maarufu wa “Time to Say Goodbye”, hatua iliyozidi kuashiria uwezekano wa yeye kufunga rasmi ukurasa wa kuchezea taifa lake.
Ishara hizo zimeongeza uzito wa taarifa kuwa huenda staa huyo mwenye umri wa miaka 37 akatangaza kustaafu soka la kimataifa muda wowote kuanzia sasa, baada ya kuitumikia Poland kwa kipindi kirefu na mafanikio makubwa binafsi.
Katika historia yake na timu ya taifa, Lewandowski ameichezea Poland katika fainali za Kombe la Dunia mara mbili, mwaka 2018 na 2022, huku akifanikiwa kufunga mabao mawili kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.
Akiwa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Poland kwa mabao 89, hakuna shaka kuwa Lewandowski ameacha alama isiyofutika. Hata hivyo, kwa wengi, haikuwa namna bora ya kusema kwaheri kwa gwiji huyo wa soka la kimataifa.


