Kambi ya timu ya taifa ya Argentina imepata afueni baada ya kubainika kuwa jeraha la nahodha wao, Lionel Messi, si kubwa kama ilivyokuwa ikihofiwa awali. Messi aliwaacha mashabiki na taharuki baada ya kuonekana akichechemea wakati akitoka uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS) uliochezwa Jumapili, Mei 24, 2026.
Nyota huyo wa Inter Miami CF alipata maumivu ya misuli ya paja katika ushindi wa mabao 6-4 dhidi ya Philadelphia Union, hali iliyozua hofu kuhusu uwezekano wa kuukosa michuano ijayo ya kimataifa pamoja na mechi muhimu za klabu yake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kupitia taarifa rasmi, Inter Miami CF imethibitisha kuwa vipimo vya kitabibu vilionyesha Messi hana mpasuko wa misuli kama ilivyodhaniwa, bali anakabiliwa na uchovu mkubwa wa misuli katika paja lake la kushoto. “Muda wa kurejea kwake uwanjani utategemea namna mwili wake utakavyoendelea kuimarika siku hadi siku chini ya usimamizi wa madaktari,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Habari hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa ndani ya kambi ya Argentina pamoja na mashabiki wa soka duniani, hasa ikizingatiwa umuhimu wa Messi katika kikosi hicho. Nahodha huyo mwenye uzoefu mkubwa anaendelea kuwa tegemeo muhimu kwa taifa lake na klabu yake licha ya umri wake kusonga mbele.
Kwa sasa, kusimama kwa michezo ya Major League Soccer kutokana na ratiba ya michuano mikubwa ya kimataifa kunatajwa kuwa faida kwa Messi, kwani atapata muda wa kutosha wa kupumzika na kurejea katika hali nzuri ya ushindani bila kulazimika kuharakishwa kurejea dimbani.


