Kocha wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel, ameweka wazi kuwa beki wa Manchester United, Harry Maguire, anakabiliwa na wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha Kombe la Dunia 2026.
Akizungumza baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Uruguay, Tuchel alifichua kuwa Maguire kwa sasa ni chaguo la tano katika safu ya ulinzi wa kati. “Kwa sasa anaangukia nafasi ya tano kutokana na ushindani uliopo,” alinukuliwa akisema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo aliwataja mabeki wanaopewa kipaumbele kuwa ni John Stones wa Manchester City, Marc Guéhi, Ezri Konsa wa Aston Villa na Trevoh Chalobah wa Chelsea, akisisitiza kuwa wanakidhi zaidi mahitaji ya mfumo wake wa sasa.
Hata hivyo, Tuchel alimuweka John Stones katika nafasi ya kipekee, akimtaja kama mchezaji wa kiwango cha dunia anayestahili kuitwa hata anapokosa muda wa kucheza klabuni. “Ana ‘credit in the bank’, ni mchezaji ninayemuamini hata katika mazingira magumu,” alieleza.
Licha ya kumpa sifa Maguire kwa utulivu wake na uwezo wa mipira ya adhabu, Tuchel alisisitiza kuwa kwa sasa anahitaji zaidi mabeki wenye kasi na uwezo wa kuendana na mfumo wake. “Ninaheshimu ubora wake kwenye set-pieces, lakini mfumo wangu unahitaji kasi zaidi,” alisema.
Aidha, Tuchel alikiri kuwa uwepo wa Maguire kwenye kikosi cha sasa umechangiwa na majeraha ya wachezaji wengine, akidokeza kuwa bila hali hiyo, huenda beki huyo mwenye miaka 33 angekosa kabisa nafasi. “Bila majeraha, ushindani ungekuwa mgumu zaidi kwake,” aliongeza, kauli inayotia shaka mustakabali wake kuelekea Kombe la Dunia.


