Mashabiki wa Iran Wakatazwa Kuingia Uwanja Mchezo Dhidi ya Egypt

Mechi ya kati ya Egypt na Iran inatarajiwa kuchezwa chini ya ulinzi mkali na katika mazingira yasiyo ya kawaida huko Seattle, Marekani, huku mjadala mkubwa ukiendelea kuhusu vikwazo vya kiusalama na kisiasa vinavyoathiri mashabiki wa Iran.

Mashabiki wa Iran Wakatazwa Kuingia Uwanja Mchezo Dhidi ya EgyptKwa mujibu wa ripoti ya NBC News, mashabiki wa Iran hawataruhusiwa kuingia uwanjani kutokana na vikwazo vya viza vilivyowekwa na serikali ya Marekani. Chanzo hicho kimenukuliwa kikisema: “Hali ya uhamiaji imeathiri moja kwa moja ushiriki wa mashabiki wa Iran katika michuano hiyo ya kimataifa.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hatua hiyo inamaanisha kuwa uwanja wa Lumen Field unaweza kushuhudia mazingira yasiyo ya kawaida, ambapo mashabiki wa Misri pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia kushangilia timu yao, hali inayoweza kubadilisha kabisa taswira ya mchezo huo muhimu wa kimataifa.

Mashabiki wa Iran Wakatazwa Kuingia Uwanja Mchezo Dhidi ya EgyptShirikisho la Soka la Iran limethibitisha kuwa mgawo wake wa tiketi ulifutwa siku chache kabla ya mchezo kupigwa Jumamosi, Juni 27, 2026. Taarifa yao imesema: “Hatua hii imetuchukulia muda mfupi na imeathiri maandalizi ya mashabiki wetu waliotarajia kusafiri.”

Mashabiki wa Iran Wakatazwa Kuingia Uwanja Mchezo Dhidi ya EgyptKwa upande wake, shirikisho la soka duniani limeeleza kuwa wachezaji wa Iran bado wataruhusiwa kushiriki, lakini kwa masharti maalum ya kuingia na kutoka Marekani siku ya mechi, wakitokea Mexico. Hali hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu usawa na haki katika mashindano ya kimataifa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.