Nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé, amefunguka kuhusu rafiki yake na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Paris Saint-Germain, Neymar Jr, kuelekea michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Mbappé amesisitiza kuwa mashindano hayo makubwa ya kombe la Dunia yanahitaji uwepo wa wachezaji wakubwa, akimtaja Neymar kuwa miongoni mwa mastaa ambao hawawezi kukosekana kwenye jukwaa hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Neymar ni Neymar, atakuwepo! Siwezi kufikiria Kombe la Dunia 2026 bila yeye,” alisema Mbappé, akionyesha imani kubwa juu ya uwezo wa nyota huyo wa Brazil kurejea katika ubora wake.
Mbali na hilo, Mbappé ameongeza kuwa ana uhakika Neymar atajiandaa vizuri na kurejea akiwa fiti licha ya changamoto za majeraha ambazo zimekuwa zikimkumba katika kipindi cha hivi karibuni.
“Nina uhakika atakuwa tayari kupambana na kuonyesha kiwango chake bora,” aliongeza Mbappé, akisisitiza umuhimu wa uzoefu na ubunifu wa Neymar kwenye mashindano makubwa.
Kauli hiyo inaonyesha jinsi Mbappé anavyothamini mchango wa Neymar, akiamini kuwa ‘uchawi’ wake bado unahitajika katika soka la kimataifa, hasa kwenye Kombe la Dunia lijalo.

