Timu ya taifa ya England imekumbwa na pigo kubwa kuelekea mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Dunia 2026 baada ya sehemu kubwa ya vifaa vya timu kuibwa nchini Marekani. Tukio hilo limetokea jijini Kansas City wakati mizigo ya timu hiyo ikisafirishwa kutoka Florida kuelekea kwenye kambi yao ya mazoezi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, vitu vilivyoibwa vinajumuisha viatu vya mechi vya baadhi ya nyota wa timu hiyo akiwemo Harry Kane na Jude Bellingham, pamoja na vifaa mbalimbali vya mazoezi vinavyotumiwa na wachezaji katika maandalizi yao ya mashindano hayo makubwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mbali na vifaa vya wachezaji, wezi hao pia waliondoka na vifaa vya benchi la ufundi, ikiwemo vifaa vya wakufunzi, mipira ya mechi na ya mashindano pamoja na sare zilizokuwa zimeandaliwa kutumika siku za michezo. Inaelezwa kuwa wizi huo ulifanyika ndani ya lori lililokuwa likisafirisha mizigo ya timu hiyo.
Baada ya tukio hilo, uongozi wa England umeanza kushirikiana kwa karibu na polisi wa Kansas City ili kuhakikisha vifaa hivyo vinapatikana au mbadala wake unapatikana kwa haraka. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha ratiba ya maandalizi ya timu chini ya kocha Thomas Tuchel haiathiriki kabla ya kuanza kwa kampeni yao ya Kombe la Dunia.
Wakati huo huo, polisi wa Kansas City wamethibitisha kuwashikilia watu wawili kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo. England inatarajiwa kuwasili Kansas City na kuanza mazoezi rasmi hivi karibuni kabla ya kushuka dimbani dhidi ya Croatia katika mchezo wao wa kwanza utakaochezwa Juni 17, 2026.


