Nyota wa Santos na timu ya taifa ya Brazil , Neymar amepata jeraha dogo la ndama lakini anatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Brazil wiki ijayo kuelekea michuano ya 2026 FIFA World Cup itakayoanza Juni 11 nchini Marekani, Canada na Mexico.
Neymar mwenye miaka 34, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Brazil, alitajwa kwenye kikosi cha taifa hilo Jumatatu baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyomkosesha sehemu kubwa ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti alikuwa kwenye presha kubwa kabla ya kutangaza kikosi hicho huku wengi wakisubiri kuona kama angemjumuisha Neymar ambaye hajacheza mechi za kimataifa tangu mwaka 2023.
Ancelotti, aliyekabidhiwa jukumu la kuinoa Brazil mwaka jana, awali alikuwa hajamrejesha mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain ambaye sasa anakipiga Santos.
Madaktari wa Santos wameeleza kuwa maendeleo ya Neymar yanaonyesha ataweza kuwa tayari kwa kambi ya timu ya taifa wiki ijayo licha ya jeraha hilo dogo.
“Neymar ana jeraha dogo la ndama, uvimbe mdogo wa misuli,” alisema mkuu wa huduma za tiba wa Santos, Rodrigo Zogaib.
“Lakini kulingana na mipango yetu, maendeleo yake yatawezesha kuwa fiti wiki ijayo atakapoungana na timu ya taifa,” aliongeza.
Neymar ambaye ana mabao 79 katika mechi 128 za kimataifa bado anakosolewa kuhusu kiwango chake na utimamu wa mwili baada ya kipindi kigumu akiwa Al Hilal kilichoathiriwa na majeraha.
Brazil itaanza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa kucheza dhidi ya Morocco Juni 13 mjini New Jersey kabla ya kukutana na Haiti na Scotland katika Kundi C.


