Mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr, amewasili kambini nchini Marekani kwa mtindo wa kipekee baada ya kutumia helikopta maarufu kama ‘Chopa’, tayari kwa maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Brazil imeweka kambi katika kituo cha Columbia Park Training Facility kilichopo Morris Township, New Jersey, ambacho hutumiwa pia na klabu ya New York Red Bulls ya Ligi Kuu Marekani (MLS).
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kuwasili kwa staa huyo kulizua gumzo kubwa kambini hapo huku akipokelewa kwa furaha na kocha mpya wa Brazil, Carlo Ancelotti, pamoja na wachezaji wenzake waliokuwa tayari wameanza mazoezi tangu mapema wiki hii. Mashabiki waliokuwa eneo hilo walionekana kuvutiwa na namna Neymar alivyoingia kambini kwa usafiri huo wa kifahari.
“Tunafurahia kumuona Neymar akiwa sehemu ya kikosi, uwepo wake unaongeza morali kubwa kwa timu,” kilieleza chanzo cha karibu na benchi la ufundi la Brazil baada ya kuwasili kwa mshambuliaji huyo mwenye uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa.
Hata hivyo, taarifa kutoka kambini zinaeleza kuwa Neymar hataanza mazoezi mazito mara moja kutokana na kusumbuliwa na jeraha dogo la misuli ya paja. Madaktari wa timu hiyo wameendelea kufanya vipimo zaidi vya kitabibu ili kufuatilia maendeleo ya nyota huyo kabla ya kumpa ruhusa ya kurejea kwenye mazoezi ya kawaida.
Kutokana na hali hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa Neymar kuukosa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 ambapo Brazil itachuana na Morocco. “Hatutaki kufanya haraka kuhusu afya yake, muhimu ni kuhakikisha anakuwa fiti kwa mechi zinazofuata,” kiliongeza chanzo hicho huku mashabiki wa Brazil wakisubiri kwa hamu taarifa rasmi kuhusu hali yake.


