Mshambuliaji wa Santos na nyota wa Brazil, Neymar Jr, ametangaza rasmi kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Brazil, akisema muda wake wa kuitumikia nchi yake umefikia tamati baada ya miaka mingi ya mafanikio na kujitoa uwanjani.
Neymar, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichoshiriki michuano ya Dunia 2026, amesema ametoa kila kitu kwa ajili ya taifa lake na sasa anaamini ni wakati mwafaka wa kufunga ukurasa huo na kuelekeza nguvu zake katika hatua nyingine ya maisha yake ya soka.
mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu
“Muda wangu na timu ya taifa umeisha. Ninaamini nimeandika historia huko, na nilifurahia kila wakati. Nimepitia mengi, nimetoa damu, jasho na maisha yangu kwa ajili ya jezi ya njano, lakini sasa nahisi sitaki kuendelea tena,” amesema Neymar.
Nyota huyo anaondoka akiwa mmoja wa wachezaji walioweka alama kubwa katika historia ya soka la Brazil, kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya timu ya taifa kwa zaidi ya muongo mmoja.
Katika kipindi chake cha kuitumikia Brazil, Neymar amecheza mechi 130, akifunga mabao 80 na kutoa asisti 59, rekodi zinazomweka miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kuvaa jezi ya taifa hilo.


