Ronaldo Ataka Mashabiki Wanaodhihaki Kifo cha Jota Kufungiwa Maisha

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ameitaka ligi ya Saudi Arabia kuchukua hatua kali dhidi ya mashabiki waliotoa nyimbo za kumdhihaki kiungo wa Al Hilal, Ruben Neves, kuhusu kifo cha rafiki yake na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Ureno, Diogo Jota.

Ronaldo Ataka Mashabiki Wanaodhihaki Kifo cha Jota Kufungiwa MaishaTukio hilo lilitokea Jumamosi wakati Al Hilal ikiibuka na ushindi mkubwa wa mabao 6-0 dhidi ya Al Taawon ugenini. Baadhi ya mashabiki walionekana kuimba nyimbo zinazohusiana na Jota, mshambuliaji wa Liverpool na Ureno aliyefariki katika ajali ya gari nchini Hispania mwaka 2025.

Ronaldo, ambaye kwa sasa anaichezea Al Nassr, alilaani kitendo hicho kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusisitiza kuwa mashabiki watakaobainika kuhusika wanapaswa kuchukuliwa hatua kali ili kuzuia vitendo kama hivyo kwenye viwanja vya soka.

“Ligi inapaswa kuchukua hatua na kuwaadhibu mashabiki wa aina hii. Watu wanaofanya mambo kama haya hawapaswi kuruhusiwa tena kuingia uwanjani,” Ronaldo aliandika.

Ronaldo Ataka Mashabiki Wanaodhihaki Kifo cha Jota Kufungiwa MaishaNeves, ambaye alikuwa mmoja wa marafiki wa karibu zaidi wa Jota na pia alihudhuria mazishi yake kama mmoja wa waliobeba jeneza, alionekana kujibu kwa kupiga makofi na kutoa ishara ya kidole gumba kwa kejeli, kabla ya kuelekeza mkono wake juu angani.

Baada ya mchezo huo, Neves alieleza kukerwa na tukio hilo akisema: “Natumaini tu hawataenda kuswali baadaye baada ya kile walichofanya.” Jota alifariki akiwa na umri wa miaka 28 pamoja na kaka yake André, mwenye miaka 25, katika ajali ya gari iliyotokea Hispania Julai 2025.

Ronaldo Ataka Mashabiki Wanaodhihaki Kifo cha Jota Kufungiwa MaishaShirikisho la Soka la Saudi Arabia pamoja na Ligi Kuu ya Saudi Arabia zilitoa taarifa ya pamoja kulaani vitendo hivyo, vikisema kamati husika tayari zimebaini waliohusika na zitachukua hatua kwa mujibu wa kanuni. Saudi Arabia, ambayo itaandaa Kombe la Dunia 2034, imewekeza kwa kiasi kikubwa katika soka na kuvutia mastaa mbalimbali akiwemo Ronaldo, Neymar na Karim Benzema.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.