Serengeti Boys Kupambana na Senegal Fainali ya AFCON U17

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U17) baada ya kuiondoa Misri kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa Mei 28, 2026 mjini Rabat, Morocco.

Serengeti Boys Kupambana na Senegal Fainali ya AFCON U17 Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 kabla ya Tanzania kuibuka mshindi kupitia changamoto ya mikwaju ya penalti.“Serengeti Boys wameonyesha uthubutu mkubwa na nidhamu ya hali ya juu katika mashindano haya, jambo lililowafanya kufika hatua ya mwisho ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika,” ilieleza taarifa baada ya ushindi huo wa kihistoria dhidi ya Misri.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika hatua ya fainali, Tanzania sasa itakutana na Senegal ambao walitinga hatua hiyo baada ya kuwatoa wenyeji Morocco kwa ushindi wa penalti 7-6 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya muda wa kawaida. Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumanne, Juni 2, 2026 katika jiji la Rabat nchini Morocco.

Serengeti Boys Kupambana na Senegal Fainali ya AFCON U17 Safari ya Serengeti Boys kuelekea fainali imekuwa ya kuvutia baada ya kuongoza kundi C kabla ya kuitoa Algeria katika robo fainali na baadaye kuichapa Misri kwenye nusu fainali. Kwa upande wa Senegal, wao waliongoza kundi D na kuiondoa Mali katika hatua ya robo fainali kabla ya ushindi wao dhidi ya Morocco.

Serengeti Boys Kupambana na Senegal Fainali ya AFCON U17 Mbali na kuwania ubingwa wa Afrika, Tanzania na Senegal tayari zimejihakikishia nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika Qatar mwishoni mwa Novemba na mwanzoni mwa Desemba mwaka huu. Mataifa mengine ya Afrika yatakayoshiriki michuano hiyo ni pamoja na Morocco, Misri, Mali, Ivory Coast, Algeria, Cameroon, Uganda na Msumbiji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.